Biden awapunguzia adhabu wafungwa 2,500 wa dawa za kulevya wasio na vurugu
HABARI
Published on 18/01/2025
Biden awapunguzia adhabu wafungwa 2,500 wa dawa za kulevya wasio na vurugu
Rais wa Marekani Joe Biden amepunguzia adhabu ya wafungwa 2,500 waliokuwa wamehukumiwa vifungo virefu kutokana makosa yanayohusisha dawa za kulevya, siku tatu kabla ya kuondoka madarakani.
Biden amesema wafungwa walikuwa wanatumikia vifungo vya muda mrefu kinyume na hukumu zinazotolea katika sheria inayotumika sasa na uamuzi wake ungesahihisha "makosa ya kihistoria".
Katika tangazo alilolitangaza leo siku ya Ijumaa Biden amesamehea na kupunguzia adhabu wafungwa wengi kuliko watangulizi wake katika historia ya Marekani.
Habari hii inakuja baada ya rais anayemaliza muda wake kupunguza vifungo vya wafungwa 37 kati ya 40 wa kifungo cha kifo, na kutoa msamaha na kupunguza vifungo kwa wingi mwezi Desemba, ikiwa ni pamoja na kwa mtoto wake, Hunter Biden.
Wakati akiwa Seneta wa Marekani, Biden alikusudia sheria ya mwaka 1986 ambayo iliweka utofauti huu wa vifungo, lakini alikubaliana kuondoa mwongozo huo, jambo lililotimia mwaka 2022.
Mabadiliko ya mtazamo wa rais baada ya miongo kadhaa akiwa mtumishi wa umma yanaonyesha jinsi mitazamo kuhusu “vita dhidi ya dawa za kulevya” nchini Marekani - ambavyo viliona vifungo vikali vikiwekwa kwa makosa ya dawa, hasa kwa wachache wa kikabila, kuanzia miaka ya 1970 - imebadilika.
“Hatua hii ni hatua muhimu kuelekea kurekebisha makosa ya kihistoria, kusawazisha utofauti wa vifungo, na kutoa fursa kwa watu wanaostahili kurudi kwa familia zao na jamii zao baada ya kutumia muda mrefu sana wakiwa gerezani,” alisema rais Ijumaa.
“Najivunia rekodi yangu ya msamaha na nitaendelea kupitia maombi ya kupunguza vifungo na kutoa msamaha.”
Comments
Comment sent successfully!