mamia ya wafungwa wametoroka katika jela
HABARI
Published on 28/01/2025
Shirika la habari la AFP linaripoti kuwa mamia ya wafungwa wametoroka katika jela moja iliyoko kwenye mji wa #goma, saa chache baada ya kuripotiwa kuwa waasi wa #M23 na wanajeshi wa #Rwanda, wameingia kwenye baadhi ya maeneo ya mji wa Goma.
Vyanzo vilivyonukuliwa na shirika hilo, vinadai kuwa gereza hilo lilikuwa na uwezo wa kuhifadhi wafungwa elfu 3, na kwamba miundombinu yake ilichomwa moto, bila hata hivyo vyanzo hivyo vya usalama kueleza kwa kina kilichojiri.
Haya yanaripotiwa wakati huu Serikali ya Rwanda ikisema imetuma mabasi kwenye mpaka wa nchi hiyo na #DRC kwa ajili ya kuwaondoa wafanyakazi wa umoja wa Mataifa.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi toka kwa Serikali ya Congo kuhusu kinachoendelea kwenye mji huo.
Slava media inaendelea kufuatilia kwa karibu kukusanya taarifa ya kinachojiri kwa sasa.
Comments
Comment sent successfully!