Iran yawanyonga watu 901 mwaka 2024 - UN
HABARI
Published on 07/01/2025

Takribani watu 901 wamenyongwa nchini Iran mwaka jana, wakiwemo 40 ndani ya wiki moja mwezi Disemba, kulingana na mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

"Inasikitisha sana bado tunaona idadi kubwa ya watu wanaokabiliwa na hukumu ya kifo nchini Iran mwaka hadi mwaka," amesema Volker Türk. "Ni wakati muafaka Iran kukomesha wimbi hili la kunyonga."

Ni kiwango kubwa zaidi kurekodiwa katika miaka tisa iliyopita na ongezeko la 6% kutoka 2023, mwaka ambao watu 853 waliuawa.

Wengi wa walionyongwa yalikuwa ya makosa yanayohusiana na dawa za kulevya, pia wapinzani na watu waliohusishwa na maandamano ya 2022 walinyongwa, kulingana na UN. Vilevile kulikuwa na ongezeko la idadi ya wanawake walionyongwa, wakifikia 31.

Türk ameitaka Iran kusitisha unyongaji na kusitisha matumizi ya hukumu ya kifo kwa nia ya kukomesha kabisa hukumu hiyo.

Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa aliwaambia waandishi wa habari kwamba takwimu hizo zimetoka kutoka mashirika kadhaa ambayo inaamini yako huru, likiwemo Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu la Iran (HRANA), Shirika la Haki za Binadamu la Iran (IHR) na Hengaw.

 

Comments
Comment sent successfully!