Rais William Ruto amewakejeli wanaopinga mpango wa chanjo ya mifugo uliopangwa kuanza Januari, 2025.
Rais Ruto amesema kuwa mpango huo utaimarisha wakulima ili kuendana na viwango vya kimataifa wakati wa kuuza bidhaa za nyama na ngozi nje ya nchi.
Ruto amewataka wanasiasa wanaopinga mpango huo kuacha kueneza propaganda.
"Chanjo inatolewa hata kwa binadamu. Ikiwa sio hatari kuwachanja watu kwa nini iwe hatari kuwachanja wanyama?", William Ruto ameuliza.
Hata hivyo, kuna baadhi ya wafugaji ambao wanapinga chanjo ya hiyo wakidai kuwa hawakupewa taarifa mapema huku wakiitaka serikali kutoa maelezo kamili kuhusu zoezi hilo.
Chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa kwa ng’ombe milioni 20 dhidi ya Ugonjwa wa Miguu na Midomo na kondoo na mbuzi milioni 50 kote nchini Kenya