MABORESHO YA UTUKUFU FM YAFUNGUA FURSA KWA WAFANYA BIASHARA
HABARI
Published on 09/12/2024
Kampuni ya UTUKUFU MEDIA GROUP CO.LTD. Ambayo ndiye mmiliki mkubwa wa Utukufu Media na Utukufu Fm, Wanapenda kuwatangazia wasikilizaji wetu na wanaofatilia mitandao yetu ya kijamii kuwa Kampuni imefanya maboresho katika sehemu zifuatazo:
1. Maboresho kwenye nembo ambayo ilikuwa inatumika hapo awali ambapo kwasasa KItuo cha utukufu Fm na Utukufu Media watatumia Nembo Hiyo kama Ishara ya kuwakilisha kituo chetu cha utukufu fm.
2. Maboresho katika Upande wa maudhui ya vipindi mwanzoni kituo chetu kilikuwa kikifanya matangazo yake katika mfumo wa maudhui ya Kidini, sasa kituo chetu kitaanza ufanya matangazo yake kwa maudhui yote, nyimbo zote zitaruhusiwa kupigwa kwenye kituo chetu. ikiwemo bongo flavour, Rhumba, Twist, Nanchi, Slow, Country songs na mengine.
3. Maboresho kwenye Kauri Mbiu ya Kituo, Mwanzoni ilitumika INJILI ISIYOGOSHIWA, kama Kauli mbiu ya kituo hiki, lakini sasa itatumika "THIS IS HOW WE LIVE" IKiwa na maana hivi ndivo tunavyoishi.
Baada ya hayo pia Utukufu Fm na Utukufu Media, Tumeboresha kwenye majukwaa ambayo tunasikika (Streaming Platforms)
Ambapo kwa sasa Radio ya Utukufu Fm itasikika kwenye majukwaa yafuatayo:
- Kwenye WEbsite ya www.utukufufm.com
- Lakini pia kupitia Application yetu ambayo kwasasa ipo:
1. Google PLaystore
2. Google appstore
3. iOs
4. Web apps
5. PC
Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu kwa Sapoti kubwa ambayo munaendelea kuionyesha kwetu, na tunathamini kila Maoni ambayo mmekuwa mkiyawakilisha kwetu kila siku kupitia Ukurasa wa maoni (Comment Section) kwenye website yetu. TUnaom,ba muendelee kutusapoti na sisi tunaahidi kuwapa Burudani, Elimu, pamoja na Kuwahabarisha kila sekunde habari mbali mbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi, michezo na Burudani, hasahasa kwenye Sport's Corner ya Utukufu fm.
Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Utukufu Media
Elikana Felix Batona
Comments
Comment sent successfully!