Mwanamuziki Chris Brown anasema anaishtaki studio ya filamu kutokana na filamu iliyotolewa mwaka jana ambayo ilijumuisha tuhuma za unyanyasaji wa kingono.
Filamu ya ‘Chris Brown: A History of Violence’ ilitolewa na Warner Bros mnamo mwezi Oktoba na iliangazia ushuhuda kutoka kwa mcheza densi ambaye jina lake halikutajwa aliyedai kuwa alimbaka kwenye boti mnamo mwaka 2020.
Katika taarifa, mawakili wa mwimbaji huyo wanasema filamu hiyo ni "ya kukashifu", na madai yake "hayakuwa na msingi" na yenye "hisia", wakimtuhumu Warner Bros kwa "kuharibu" sifa yake bila kujali.
Pamoja na Warner Bros, kesi hiyo pia inataja kampuni ya Ample. Hakuna iliyojibu ilipotafutwa kwa maoni na BBC Newsbeat.