HABARI ZA MICHEZO KIMATAIFA
MICHEZO
Published on 18/12/2024

Atletico Madrid wanafikiria kumnunua winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho Januari, (Fichajes - In Spanish)

Manchester United wako kwenye mazungumzo ya hali ya juu ili kuongeza mkataba wa winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 22, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika msimu ujao. (ESPN)

Mkufunzi wa Roma Claudio Ranieri anasema fowadi wa Argentina Paulo Dybala, 31, anaweza kuondoka katika klabu hiyo ikiwa hana furaha, baada ya wakala wake kukutana na Galatasaray. (Corriere dello Sport - In Italy)

Manchester United wanaweza kupambana na RB Leipzig inayoshiriki Bundesliga kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, kwa mkopo mwezi Januari. (Football Insider)

Chelsea, Aston Villa, Stuttgart na Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa kimataifa wa PAOK na Ugiriki chini ya umri wa miaka 21 Stefanos Tzimas, 18 ambaye amecheza kwa mkopo Nurnberg. (ESPN)

Mazungumzo bado yanaendelea kati ya Southampton na mkufunzi wa Sheffield Wednesday Danny Rohl kuhusu nafasi ya ukocha katika klabu ya St Mary's. (Sky Germany)

Saints pia wanamfikiria kocha mkuu wa West Brom Carlos Corberan kama mgombeaji. (Sky Sports)

West Ham wamekuwa wakimsaka kipa wa Freiburg Mjerumani mwenye umri wa miaka 22 Noah Atubolu. (Fabrizio Romano)

Burnley wako kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumsajili beki wa kulia wa Peru Oliver Sonne, 24, kutoka Silkeborg kwa mkataba wa thamani ya £2.5m. (Football Insider)

Kocha wa zamani wa Birmingham City na Millwall Gary Rowett yuko kwenye mazungumzo ya kina na Oxford United kuhusu nafasi yao ya ukocha. (John Percy/Telegraph)

Barcelona imewaonya mlinzi wa Uruguay Ronald Araujo, 25, na kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 27, kusaini mikataba mipya katika klabu hiyo la sivyo wakabiliwe na uwezekano wa kuorodheshwa kuhama. (Sport - In Spanish)

Everton inamfuatilia mshambuliaji wa Rangers na Morocco Hamzane Igamane, 22, huku mustakabali wa mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 27, na mshambuliaji wa Ureno Beto, 26, katika klabu hiyo haueleweki. (TBR Football)

Juventus wanapanga kumnunua mlinzi wa Feyenoord na Slovakia David Hancko, 27, huku timu hiyo ya Italia ikijaribu kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Calciomercato - In Italy)

 

 

Comments
Comment sent successfully!