HABARI ZA MICHEZO ULAYA 23/10/2024
MICHEZO
Published on 23/10/2024

 

Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi amefanya mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kuchukua nafasi ya Erik ten Hag.

Sevilla wana nia ya kumsajili beki wa Tottenham mwenye umri wa miaka 18, Archie Gray kwa mkopo.

 

Chelsea imemwambia mlinzi wa umri wa miaka 18 wa England Josh Acheampong kwamba hataichezea klabu hiyo kwa kiwango chochote tena hadi asaini mkataba mpya. (Athletic - Usajili unahitajika)

 

 

Tottenham wameweka bei ya pauni milioni 80 kwa beki wa Uhispania Pedro Porro, 25, ambaye anawindwa na Manchester City. (Football Insider)

 

Brighton na Arsenal wanavutiwa na kipa wa Aston Villa wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 21 raia wa Poland Oliwier Zych. (Telegraph - usajili unahitajika)

 

Kocha wa Arsenal wa timu ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 18 Jack Wilshere, 32, atajiunga na Norwich kama mkufunzi wa kikosi cha kwanza wiki hii baada ya klabu hizo mbili kukubaliana ada ya fidia kwa kiungo huyo wa zamani wa Gunners.

 

Graham Potter, David Moyes na Gareth Southgate wanatarajiwa kurithi mikoba ya Oliver Glasner iwapo atatimuliwa na Crystal Palace. (Guardian)

 

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Edin Terzic atawania kazi katika klabu ya West Ham iwapo The Hammers watamfukuza Julen Lopetegui. (Florian Plettenberg)

 

Dortmund wanataka kumsajili beki mwezi Januari huku mchezaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 Ben Chilwell na mchezaji wa kimataifa wa Hungary na Bournemouth Milos Kerkez, 20, wakijumuishwa kwenye orodha yao fupi. (Team Talk)

 

Wachezaji wakuu barani Ulaya henda wakakataa kutangaza Kombe la Dunia la Vilabu lililopanuliwa hivi karibuni kama sehemu ya mzozo kati ya vyama vya wachezaji na Fifa kuhusu kalenda ya soka iliyosongamana. (Times- usajili unahitajika)

 

Mpango wa Freidkin Group wa kuinunua klabu ya Everton unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba, lakini wamiliki hao wapya hawataidhinisha matumizi makubwa ya Januari kwa sababu ya vikwazo vya PSR. (The i - Usajili unahitajika)

 

Israel yasema ilimuua aliyetarajiwa kumrithi Nasrallah

Comments
Comment sent successfully!