Trump ashtaki gazeti kwa 'kuingilia uchaguzi'
SIASA
Published on 18/12/2024

Rais mteule Donald Trump ameshtaki gazeti la Des Moines Register, pamoja na kampuni yake mama na mchanganuzi wake wa zamani, kwa "kuingilia kati uchaguzi" juu ya kura ya maoni iliyochapishwa siku chache kabla ya uchaguzi wa rais wa 2024.

Kura ya maoni ya Novemba 2 ilipendekeza mgombeaji wa chama cha Democratic Kamala Harris angeshinda jimbo la Iowa, lenye watu wengi wa chama cha Republican.

Trump aliwasilisha kesi hiyo mpya baada ya kushinda kesi dhidi ya shirika la habari la ABC News kwa kumchafulia jina akifidiwa $15m (£12m), juu ya mtangazaji aliyesema uwongo kuwa Trump alipatikana na hatia ya ubakaji mwaka jana.

Mtazamo wa mara kwa mara wa Trump kwa vyombo vya habari vya Marekani unarejelea kampeni yake ya kwanza ya urais, na anatarajiwa kuendelea hadi muhula wake wa pili.

Alitangaza mipango yake ya kushtaki jarida hilo lenye makao yake makuu Iowa wakati wa mkutano na wanahabari siku ya Jumatatu ambapo aliviita vyombo vya habari kuwa "vifisadi". Kesi hiyo iliwasilishwa katika Kaunti ya Polk, Iowa, baadaye asubuhi hiyo.

Katika uchaguzi huo chini ya wiki moja baadaye, Trump aliongoza katika jimbo la Iowa kwa pointi 13.

"Kwa maoni yangu, ulikuwa udanganyifu na ulikuwa uingiliaji wa uchaguzi," Trump alisema.

"Ninahisi lazima nifanye hivi," aliongeza. "Inagharimu pesa nyingi lakini inabidi tunyooshe vyombo vya habari."

 

Comments
Comment sent successfully!