Jeshi la Sudan laapa kuendelea kupigana licha ya juhudi za amani
HABARI
Published on 03/10/2024

Jenerali wa ngazi ya juu wa Sudan amesema jeshi litaendelea na mashambulizi yake licha ya juhudi za kimataifa za kukomesha mapigano katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 17.

"Mazungumzo ya amani yanaweza kuendelea, lakini jeshi halitasitisha shughuli zake kwa sababu ya hilo," Msaidizi wa Kamanda Mkuu Luteni Jenerali Ibrahim Gabir aliiambia BBC.

Alikuwa akizungumza siku chache tu baada ya jeshi kuanzisha operesheni ya kuchukuwa udhibiti wa mji mkuu, Khartoum, kutoka kwa waasi wa RSF.

Pande hizo mbili zimekuwa zikipigana tangu Aprili mwaka jana, baada ya viongozi wao kufautiana kuhusu mustakabali wa nchi.

Mzozo huo umesababisha janga la kibinadamu huku zaidi ya nusu ya nchi ikikabiliwa na njaa na mamilioni ya watu kulazimika kuyahama makazi yao.

Comments
Comment sent successfully!