INSPEKTA JENERALI WA POLICE KENYA KUNYEA DEBE MIEZI 6
HABARI
Published on 14/09/2024

Jaji wa mahakama kuu Lawrence Mugambi amemhukumu kaima Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli kifungo cha miezi sita jela kwa kuidharau mahakama.

hii ni baada ya Bwana Masengeli kupuuza wito wa mahakama mara saba.

"Bwana Masengeli Ameagizwa kujisalimisha kwa kamishina mkuu wa Magereza ili kutumikia kifungo chake. Endapo atashindwa kujisalimisha gerezani, waziri wa mambo ya ndani lazima achukue hatua kuhakikishaanapelekwa gerezani kutumikia kifungo chake" Aliamuru jaji Mugambi. 

Mkuu wa polisi huyo alitakiwa kufika mahakamani kueleza hali iliyopelekea kupotea kwa watu watatu huko Kitengela, Watu hao walipotea Tarehe 19 Agosti.

By Elikana Felix @elikana_officialtz

Comments
Comment sent successfully!