Watoto 94 wa kituo Cha yatima wako hatarini kufa na njaa.
HABARI
Published on 06/09/2024

Kituo cha Kulelea Watoto Yatima kilichopo maeneo ya Msongola Jimbo la Ukonga Wilayani Ilala kinakabiliwa na Uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watoto kituoni hapo. Ambapo kwasasa inakadiliwa kuwa na watoto zaidi ya 94.

 

Changamoto hiyo imeelezwa na miongoni mwa wadau ambao wamekuwa wakisapoti sana Kituo hicho Bi. DEODATA JOSEPH MNG'ONG'O kwa Mwandishi wetu wa Utukufu Fm alipotembelea katika kituo hicho Cha habari kilichopo Gongolamboto, 

 

Aidha Bi DEODATA ameahidi kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kupunguza ukubwa wa changamoto hiyo na kutoa rai kwa yeyote mwenye kuguswa na jambo hilo kujitolea kuwasaidia watoto hao ili waweza kupata chakula cha kukidhi mahitaji yao. Lakini pia kupata pesa ya ujenzi wa eneo lao la makazi, kupata mavazi pamoja na pesa Kwa ajili ya elimu yao. "BINADAMU TUNAISHI KWA KUTEGEMEA NA HATAWEWE UNAWEZA KUWA TUMAINI LA FURAHA KWA WATOTO 94 WAKITUO CHA WATOTO YATIMA KILICHOPO MSONGOLA MKOANI DAR ES SALAAM TANZANIA.

 

WATOTO HAO WANAHITAJI NYUMBA NZURI YA KUISHI CHAKULA ELIMU NA MAVAZI ILI WAWEZE KUTIMIZA NDOTO ZAO.

 

UNAWEZA KUWA SEHEMU YA TUMAINI KWA WATOTO HAO KWA KUTUMA MCHANGO WAKO KUPITIA 

 

CRDB ACCOUNT NO, 0152 669 222 700

NMB ACCOUNT NO, 2331 0043 566

MPESA, 07 45 12 96 83

HALOPESA 06 17 23 44 43

 

ACCOUNT ZOTE HIZO JINA LITATOKEA 

DEODATA JOSEPH MNG'ONG'O

 

YAKOBO SURA YA KWANZA MSTARI WA ISHIRINI NA SABA, MANDIKO YANASEMA, NANUKUU: DINI ILIYO SAFI ISIYO NA TAKA MBELE ZA MUNGU BABA NI HII KWENDA KUWATAZAMA YATIMA NA WAJANE KATIKA DHIKI YAO,NA KUJILINDA NA DUNIA PASIPO MAWAA. 

 

MUNGU AKUZIDISHIE PALE UTAKAPO TOA" Alisema Madam DEODATA JOSEPH MNG'ONG'O

Comments
Comment sent successfully!