Mauaji ya 2009 nchini Guinea: Mawakili wa dikteta wa zamani Camara watangaza kukata rufaa
HABARI
Published on 02/08/2024
 
Mawakili wa dikteta wa zamani Moussa Dadis Camara, aliyhukumiwa siku ya Jumatano kifungo cha miaka 20 jela kwa uhalifu dhidi ya binadamu kwa kuhusika katika mauaji ya Septemba 28, 2009 nchini Guinea, wametangaza siku ya Alhamisi kwamba watakata rufaa.
"Muungano wa mawakili unakataa uamuzi huu kwa ujumla na, kuonyesha kutokubaliana kwake, kwa kukubaliana na rais Moussa Dadis Camara, kukata rufaa dhidi ya hukumu hii isiyo ya haki ili ifutwe na Mahakama ya Rufaa," muungao wa wanasheria wa Moussa Dadis Camara umesema katika taarifa yake.
"Ikumbukwe kwamba karibu miaka miwili ya kesi mbele ya mahakama hii, rais Moussa Dadis Camara hakuwahi kusikilizwa au kuhitajika kujieleza kuhusiana na uhalifu dhidi ya binadamu," muungano huo umeongeza, ukitishia kupeleka suala hilo kwenye Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
Siku ya Jumatano, wakati hukumu ya kesi ya kihistoria mjini Conakry ilipotangazwa, mashitaka yalibadilishwa na mahakama kama uhalifu dhidi ya binadamu.
Moussa Dadis Camara alipatikana na hatia "kwa msingi wa jukumu la mkuu", alitangaza Ibrahima Sory II Tounkara, jajikiongozi wa mahakama. Pia alipatikana na hatia kwa "nia yake ya kukandamiza maandamano" na kwa kushindwa katika jukumu lake la kuwaadhibu wahusika wa mauaji hayo.
Dikteta huyo wa zamani alikuwa anakabiliwa na safu ya uhalifu ikiwa ni pamoja na mauaji, unyanyasaji wa kijinsia, vitendo vya utesaji, utekaji nyara na watu kufungwa kusikojulikana. Alikuwa akikabiliwa na kifungo cha maisha.
Mnamo Septemba 28, 2009, watu wasiopungua 156 waliuawa kwa risasi, kisu na mapanga, na mamia ya wengine kujeruhiwa, katika ukandamizaji wa maandamano ya upinzani katika uwanja wa Conakry na viung vyake, kulingana na ripoti ya kimataifa ya tume ya uchunguzi iliyopewa mamlaka na Umoja wa Mataifa. Angalau wanawake 109 walibakwa.
Unyanyasaji huo, ambao takwimu halisi huenda ni kubwa zaidi, uliendelea kwa siku kadhaa dhidi ya wanawake waliotekwa nyara na wafungwa walioteswa katika kile kinachochukuliwa kuwa moja ya matukio mabaya zaidi katika historia ya sasa ya Guinea.
Comments
Comment sent successfully!