Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi Aeleza maboresho ambayo yamefanywa kwenye vipindi
HABARI
Published on 01/08/2024

Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi katika kituo Cha habari Cha UTUKUFU FM, kinachomilikiwa na Evangelism Media Group Foundation (EMGF) Taasisi ambayo Ina makao makuu yake katika jiji la Dar es salaam nchini Tanzania Bw. Elikana Felix Batona, amefafanua namna katika idara ya uzalishaji wa vipindi alivyoboresha vipindi Kwa ajili ya kuongeza Radha ya vipindi Kwa wasikilizaji, Moja katika maboresho yaliyofanyika ni pamoja na kuongeza kipindi Cha michezo kinachoitwa Sports corner ya Utukufu Fm, ambacho kinaruka Kila siku majira ya saa Moja na nusu (07h00Am) mpaka saa 08h00 asubuhi lakini pia kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 12 jioni Kila siku kuanzia juma tatu mpaka ijumaa, lakini pia juma mosi na juma pili kuanzia saa 20h00PM usiku mpaka saa 21h00. Lakini pia mbali na hayo mkurugenzi huyo amesema kuwa Kuna maongezeko ya vipindi vya Lugha ya kingereza. Kikiwemo kipindi Cha Interpreneurship Arts and decorations, ambacho kutakuwa kinaluka Kila siku ya alhamisi saa mbili asubuhi mpaka saa tatu na marudio yake saa 21h00 mpaka saa 22h00 usiku siku ya juma pili. Maboresho hayo yamefanyika Kwa kuzingatia uhitaji wa wasikilizaji wetu na kutambua umuhimu wa vipindi husika Kwa jamii yetu na Kwa ulimwengu wa Sasa ambayo unazingatia science na technolojia. Hayo aliyasema Bw. Elikana, Kwa niaba ya Utukufu News ni @journalist Royal Queen. 

Comments
Comment sent successfully!