Kumi na moja wafariki katika shambulio la roketi Israeli
HABARI
Published on 27/07/2024

Vijana 11 wameuawa huku 19 wakijeruhiwa baada ya shambulio lililotokea kwenye uwanja wa mpira wa miguu katika Milima ya Golan inayokaliwa na Israeli, kulingana na huduma za dharura za Israeli na wasemaji wa jeshi.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema roketi ilianguka kwenye eneo la Majdal Shams katika eneo hilo.

Shambulizi hilo ni baya zaidi kutokea katika eneo hilo tangu kuanza kwa makabiliano ya kurushiana risasi mpakani kati ya jeshi la Israeli na Hezbollah kuongezeka baada ya Hezbollah kurusha makombora katika maeneo ya Israeli siku moja baada ya kuzuka kwa vita vya Israel na Gaza mnamo mwezi Oktoba.

IDF ililaumu Hezbollah kwa shambulio hilo lakini msemaji wa Hezbollah Mohamad Afif, alikanusha "uhusiano wowote na tukio la Majdel Shams" kaskazini mwa Israel na shutuma zote [za kuhusika kwa kundi hilo] ni za uongo".

Wanajeshi wa Israeli na Hezbollah wamekuwa wakirushiana risasi kuvuka mpaka tangu vita vya Israeli na Hamas kuanza mnamo mwezi Oktoba

Comments
Comment sent successfully!