Rais William Ruto nchini Kenya amefanya tena mabadiliko katika baraza la mawaziri.
Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Aden Duale amepelekwa katika wizara ya mazingira huku Waziri aliyekuwa ametuliwa kushika nafasi hiyo, Soipan Tuya akipewa Wizara ya Ulinzi.
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, mheshimiwa Aden Duale alisema, ‘’Ninamshukuru Rais @WilliamsRuto kwa kunitoa kutoka Wizara ya Ulinzi hadi Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu’’.
Alionyesha kujitolea kwake katika majumu yake mapya, na kusisitiza kuwa atahakikisha angalizo linawekwa katika usimamizi endelevu wa mazingira, kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kukuza juhudi za upandaji miti na uhifadhi.
Rais William Ruto alitangaza mawaziri kumi na moja katika baraza lake la mawaziri.
Katika hotuba yake kwa taifa, rais Ruto alisema kwamba idadi ya mawaziri waliosalia itatangazwa baada ya mashauriano.
Hayo yalijiri baada ya shinikizo kuongezeka kwa Rais kuchagua watu wenye uwezo ambao watamsaidia kutekeleza ajenda yake.