Netanyahu akabiliwa na wakati mgumu baada ya Biden kujiondoa
HABARI
Published on 23/07/2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaizuru Marekani wiki huku akikabiliwa na shinikizo la kukomesha vita vya Gaza, kutoka kwa Waisraeli na utawala wa Marekani. Je, msukosuko wa kisiasa huko Washington unaweza kuathiri vipi safari na mahusiano ya siku zijazo?

Bw Netanyahu anatazamiwa kukutana na Joe Biden - ikiwa rais amepona Covid-19, na kuhutubia kikao cha pamoja cha Congress, atakuwa ni kiongozi pekee wa kigeni kufanya hivyo kwa mara ya nne.

Safari hii inampa nafasi ya kurejea Washington baada ya miezi kadhaa ya mivutano kuhusu mtazamo wake mkali wa vita, na fursa ya kujaribu kuwashawishi Waisraeli kwamba hajavuruga uhusiano na mshirika wao muhimu zaidi.

Lakini ziara hii imegubikwa na uamuzi wa Rais Biden wa kutogombea tena urais, jambo lilosababisha hali ya ya sintofahamu ya kisiasa kuhusu mshirika mwingine wa Israel katika Ikulu ya White House na pengine kuathiri mambo yaliyotarajiwa kuangaziwa katika ziara ya Bw Netanyahu.

Nyumbani hakuacha mambo yakiwa mazuri hadi alipopanda ndege kuelekea Marekani. Msururu wa maandamano ulimtaka abaki nyumbani na kushughulikia makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas ili iwaachilie mateka wa Israel.

"Mpaka atie saini mkataba ulio mezani, sioni jinsi anavyojiinua na kuvuka bahari ya Atlantiki kushughulikia machafuko ya kisiasa ya Marekani," alisema Lee Siegal, mmoja wa wanafamilia wenye ndugu waliotekwa na Hamas ambao wamejitokeza kuandamana. Kaka yake Keith mwenye umri wa miaka 65 ni mfungwa huko Gaza.

Comments
Comment sent successfully!