Kikosi cha Simba Vs El-Qanah Egypt Mechi Ya Kirafiki (22 July 2024)
Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club, itaanza msimu wake wa michezo ya kirafiki kwa kucheza dhidi ya El-Qanah kutoka Misri. Mechi hii itatimua vumbi tarehe 22 Julai 2024 katika Uwanja wa Old Suez Canal. Lengo kuu la mechi hii ni kuwapa nafasi wachezaji wapya wa Simba kuonyesha uwezo wao, pamoja na kocha mpya, Fadlu Davids, kuonyesha mbinu zake za mchezo.
Mechi hii ya kirafiki ina malengo kadhaa muhimu kwa Simba SC kuelekea msimu wa 2024/2025. Miongoni mwa malengo muhimu ya mchezo huu wa kirafiki dhidi ya El-Qanah Egypt ni pamoja na;
1. Kuwapa Nafasi Wachezaji Wapya: Simba imesajili wachezaji wapya katika dirisha hili la usajili. Mechi hii itawapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao na kujenga muunganiko mzuri na wachezaji wa zamani.
2. Mtihani wa Mbinu za Kocha Mpya: Fadlu Davids, kocha mpya wa Simba, atakuwa na nafasi ya kujaribu mbinu zake za mchezo kabla ya mechi muhimu dhidi ya Yanga SC katika ngao ya jamii. Hii itasaidia kutambua maeneo yanayohitaji kuboreshwa.
Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kusisimua na yenye ushindani mkubwa. Kwa mashabiki wa Simba SC na wapenzi wa soka kwa ujumla, huu ni mtanange usiofaa kukosa. Endelea kufuatilia habari na taarifa zaidi kuhusu mchezo huu kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.
Kikosi cha Simba Vs El-Qanah Egypt Mechi Ya Kirafiki (22 July 2024)
Ingawa kikosi kamili cha Simba SC bado hakijatangazwa rasmi, tunatarajia kuona mchanganyiko wa wachezaji wazoefu na wale wapya. Wachezaji nyota kama vile Willy Essomba Onana, Mohammed Hussen na Mzamiru Yassin wanatarajiwa kuongoza kikosi hicho.
Kikosi kinachoanza Leo dhidi ya El-Qanah: Ally Salim (1) Shomari Kapombe (12) Mohamed Hussein (15) Karaboue Chamou (2) Che malone (20) Mzamiru Yassin (19) Yusuph Kagoma (21) Edwin Balua (16) Joshua Mutale (7) Jean Charles Ahoua (10) Freddy Michael (18).
Hapa chini tumekuletea orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuunda kikosi cha Simba SC dhidi ya El-Qanah Egypt
MAGOLIKIPA
- Ayoub Lakred
- Ally Salim
- Hussein Abeli
MABEKI
- Che Fondoh Malone
- Abdulrazack Hamza
- Hussein Kazi
- Chamou Karaboue
- Shomari Kapombe
- Valentin Nouma
- Mohammed Hussein
- Israel Mwenda
VIUNGO WAKABAJI
- Augustine Okejepha
- Yusuph Kagoma
- Fabrice Ngoma
- Mzamiru Yassin
- Debora Mavambo
VIUNGO WASHAMBULIAJI
- Jean Charles Ahoua
- Kibu Denis Prosper
- Omary Omary
- Joshua Mutale
- Edwin Balua
- Ladack Chasambi
- Salehe Karabaka
WASHAMBULIAJI
- Freddy Michael Kouablan
- Valentino Mashaka
- Steven Dese Mukwala