HABARI ZA MICHEZO ULAYA
MICHEZO
Published on 26/09/2024

Liverpool wako tayari kumnunua winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 23, ikiwa mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 32, ataondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu. (Fichajes - kwa Kihispania)

Wamiliki wapya watarajiwa wa Everton, Friedkin Group wanataka kumleta kocha wa zamani wa Chelsea, Maurizio Sarri, ambaye aliondoka Lazio mwezi Machi, kama mkufunzi wao mpya. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Juventus wanatumai kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 24, hadi 2028 au 2029, ingawa mazungumzo yanaripotiwa kukwama. Vlahovic amekuwa akihusishwa na Arsenal hivi karibuni. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Dusan Vlahovic

Chanzo cha picha,EPA

Maelezo ya picha,Mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic

Manchester United bado wanamtaka beki wa Everton Jarrad Branthwaite na watafanya jaribio lingine la kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anayecheza England mwaka wa 2025. (HITC)

Beki wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 23, anaongoza orodha ya Liverpool kuchukua nafasi ya Trent Alexander-Arnold ikiwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 25, ataondoka katika klabu hiyo. (Football Insider)

Chelsea inamnyata beki wa RB Leipzig ya Ufaransa Castello Lukeba, 21, huku wakilenga kuwasajili wachezaji bora chipukizi duniani. (Teamtalk)

Mshambulizi wa Bayer Leverkusen na Nigeria Victor Boniface, 23, yuko kwenye orodha ya wamshambuliaji wapya wanaosakwa na Chelsea. (Teamtalk)

Barcelona wanamchukulia mlinda lango wa Porto wa Ureno Diogo Costa, 25, kama chaguo la muda mrefu kuchukua nafasi ya kipa wa Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 32. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Manchester United wanataka kupunguza nafasi ya wachezaji wa safu ya kati na wanaweza kuwaachia Christian Eriksen na Casemiro, 32, kuondoka Januari. (Teamtalk)

XX

Chanzo cha picha,Getty Images

Kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Mjerumani Francis Onyeka, 17, anawindwa na Chelsea. (Footbal Transfers)

Newcastle United imezishinda klabu za Real Madrid, Bayern Munich na Borussia Dortmund kupata huduma ya mshambuliaji wa Dinamo Tbilisi mwenye umri wa miaka 17 kutoka Georgia Vakhtang Salia. (HITC)

 

Comments
Comment sent successfully!