Waliofariki katika tetemeko la ardhi Tibet wafikia 126
HABARI
Published on 07/01/2025

Takribani watu 126 wamefariki, na wengine 188 wamejeruhiwa, baada ya tetemeko la ardhi kupiga vilima vya Himalaya siku ya Jumanne, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya China.

Wafanyakazi wa uokoaji wanafukua vifusi kutafuta manusura baada ya tetemeko hilo lililoharibu zaid ya majengo 1,000 katika eneo la Tibet, karibu na mlima wa Everest.

Operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea, huku walionusurika wakiwa chini ya shinikizo la ziada kwani halijoto inatabiriwa kushuka hadi nyuzijoto 16C (3.2F).

Matetemeko ya ardhi ni ya kawaida katika eneo hilo, kutokana na jiografia yake, lakini tetemeko hilo limeacha vifo vya watu wengi zaidi nchini China katika miaka ya hivi karibuni.

Tetemeko hilo la ukubwa wa 7.1, ambalo lilipiga kwa kina cha kilomita 10 (maili sita), kulingana na data kutoka Geological Survey ya Marekani, pia lilisikika nchini Nepal na nsehemu za India, ambazo ni jirani na Tibet.

 

Comments
Comment sent successfully!