Makao makuu ya Bunge yaharibiwa kwa moto, uchunguzi unaendelea
HABARI
Published on 19/12/2024
Nchini Liberia, moto umeteketeza sehemu ya jengo la Baraza la Wawakilishi mapema Jumatano, na kufaanya timu kadhaa za uokoaji kuingilia kati. Ingawa moto huo sasa umedhibitiwa, chanzo chake bado hakijajulikana. Uchunguzi unaendelea ili kubaini sababu. Tukio hili linaongeza mfululizo wa migogoro ambayo tayari inadhofisha Bunge la nchi hiyo.
Ilikuwa karibu saa 12 asubuhi kwa saa za ndani ambapo moto huo uliripotiwa katika makao maku ya Bunge la taifa huko Monrovia, mji mkuu wa Liberia, ukiambatana na mawingu ya moshi mweusi, unaoonekana kwa mbali. Video zilizoruhwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha miali ya moto ya kutisha ikiteketeza sehemu ya jengo bunge hilo.
Kulingana na mamlaka, timu za uokoaji - zilizoundwa na wazima moto wa kitaifa na huduma kadhaa za dharura zimeingilia kati- na hivyo kudhibiti moto huo na kuzuia kuenea kwa sehemu zingine za jengo.
Hakuna majeraha yaliyoripotiwa, hata hivyo ukosoaji umeibuka kuhusu uhaba wa vifaa vya wazima moto.
Mkutano kati ya rais na vikosi vya usalama
Hili sio tukio la kwanza la moto katika Bunge: siku chache zilizopita, moto mwingine ulizuka, lakini wa kiwango kidogo.
Kwa sasa, ni mapema sana kusema ikiwa sababu ya tukio hilo ilikuwa ajali au makusudi. Tukio hili linatokea katika hali ya mvutano wa kisiasa, inayoashiria mapambano makali kati ya kambi mbili zinazohasimiana kuwania uspika wa Bunge la taifa.
Mkuu wa nchi, Joseph Boakai, anafanya mkutano na vikosi vya usalama ili kujua sababu za moto huo. Taarifa rasmi inatarajiwa saa chache zijazo.