Marekani imekuwa ikiimarisha juhudi za kidiplomasia kufufua mazungumzo ya kusitisha mapigano katika Gaza na Lebanon.
Mjumbe maalumu wa rais wa Marekani nchini Lebanon, Amos Hochstein, anasema pande zote zinafanya kazi katika kutengeneza kanuni itakayomaliza mzozo wa Israel na Hezbollah "mara moja na kwa wote".
Hochstein amesema walikuwa wakijaribu kuweka mifumo ili kuwezesha pande zote kuingia katika enzi mpya ya ustawi.
"Marekani inataka kumaliza mzozo huu haraka iwezekanavyo," mjumbe anaongeza.
Alikuwa akizungumza katika mji mkuu wa Lebanon Beirut, ambako amekuwa akikutana na kiongozi mkongwe wa Shia Nabih Berri, ambaye ana jukumu la kufanya mazungumzo kwa niaba ya Hezbollah.